
KIJANA mmoja raia wa Somalia, Bashir Mohamed, ameoa wanawake wawili siku mmoja na ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) kwamba atawashawishi wanaume wengine kufanya hivyo.
Kijana huyo anasema kuwa aliwachumbia wanawake wote kwa takriban miezi minane na kuwashawishi kufunga ndoa naye.
”Nilikuwa nikiwaleta nyumbaji wote pamoja”, aliliambia BBC.
”Nilikuwa nikiwaambia wazi wote wawili kwamba nawapenda. Waliridhika” , aliongezea.
”Umuhimu wa kuwaoa wote wawili wakati mmoja ni kwamba hawangekuwa na wivu na kwamba watajua tangu awali kwamba wamekuwa katika ndoa za uke wenza”, alisema Mohammed.
Alioa wanawake wawili kwa sababu alihitaji watoto wengi.
”Nitawashawishi wanaume wengi pia kufuata nyayo zangu iwapo wana uwezo”, alisema Mohamed.
Ndoa za wake wengi ni halali katika utamaduni nchini Somalia lakini si jambo la kawaida kuoa wanawake wawili wakati mmoja, kulingana na mwandishi wa BBC, Mohamed Mohamed.
”Imetokea mara kadhaa katika miaka ya nyuma ikiashiria kwamba huenda sasa ikawa mtindo mpya”, aliongezea.
Mwanandoa huyo aliwaoa wanawake hao wawili , Iqra na Nimo, katika kijiji cha Sinai katika jimbo lililojitenga la Somaliland tarehe 22 mwezi Juni.
CREDIT: BBC SWAHILI