
Mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia Brazil watakuwa wenyeji wa Mexico Samara Arena, Samara Jumatatu tarehe 2/7/2018.
Hii ni baada ya Brazil kudondoka hadi hatua ya mchujo kwa kumaliza wa kwanza Kundi E na alama 7.
Kwa upande wake Mexico ilinyakua nafasi ya pili Kundi F baada ya Ujerumani kulemewa na Korea Kusini 2-0.
Siku itakayofuata ya Jumanne 3/7/2018, Uswizi itakuwa mgeni wa Sweden iliyotwaa nafasi ya kwanza Kundi F, ugani Krestovsky, Saint Petersburg,.

Uswizi ilijikakamua na kutoka sare 2-2 dhidi ya Costa Rica ugani Nizhny Novgorod.
Licha ya kujaribu kuipiku Uswizi nafasi ya pili, Serbia imelazimika kujituliza na nafasi ya tatu Kundi E.
Nyota wa Uswizi aliyetia kimiani goli la kwanza dhidi ya Costa Rica, Blerim Dzemaili ndiye mchezaji bora wa mechi hiyo .
Dzemaili alifungua hesabu (dakika ya 31) lakini Waston akaisawazishia Costa Rica (dakika ya 56).

Uswizi ilikaribia kusajili ushindi wa pili Urusi baada ya nguvu mpya Drmic kufunga zikiwa zimesalia dakika chache mechi kumalizaika (dakika ya 88). Ndoto hizo zilikatizwa baadaye.
Licha ya kuwa na mchezo mzuri mechini, mdakaji wa Uswizi Sommer alijifunga mwenyewe baada ya Penalti ya Ruiz (dakika ya 93).
Wawili kati ya timu hizi nne wataliaga kombe hili na kujiunga na timu 12 ambazo kwa sasa zimegeuka watazamaji baada ya kutemwa hatua ya makundi.
Serbia nje ya Kombe la Dunia
Mechi imekamilika: Serbia 0-2 Brazil.
Brazil wamemaliza wa kwanza Kundi E.
- Paulinho na goli la kwanza (Dakika ya 36)
- Thiago Silva kwa kichwa goli la pili (Dakika ya68)
Costa Rica wapachika penalti: Bryan Ruiz!
93′ Uswizi 2-2 Costa Rica