×

Lori la Mafuta Laacha Njia na Kuanguka Buguruni – Pichaz

AJALI mbaya ya lori la mafuta (oil ya kuchanganyia na diesel) limeacha njia na kupinduka katika eneo la Buguruni Sheli jijini Dar es Salaam, jioni hii ya Jumamosi, Juni 30, 2018 na kuzua taharuki miongoni mwa wakazi wa eneo hilo na wananchi waliokuwa wakipita.

Kamera ya Global Publishers iliyokuwa eneo la tukio wakati lori hilo likipinduka, imeshuhudia wananchi wakivamia huku wamebebelea madumu na ndoo kwa ajili ya kuchota oil hiyo iliyokuwa ikimwagika kutoka kwenye kontena.

Aidha, bado haijafahamika iwapo kuna majeruhi au watu waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo.

Ajali hiyo imesababisha adha kubwa hasa ya usafiri kwani kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari huku Jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi ili kuhakikisha hakuna hali ya uvunjifu wa amani wakati wa uokoaji na kulitoa gari hilo eneo la tukio.

Picha zinaonyesha tukio lilivyokuwa, kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.

Picha na Richard Bukos, Global Publishers.