×

Simba Hatari! Yawatungua Wasomali 4G

TIMU ya Msimbazi, Simba SC wameanza vema safari ya kupigania ubingwa wa michuano ya Kagame baada ya kuitandika bao 4-0 klabu ya Dakadaha kutoka Somalia.

 

Katika mchezo huo ulipigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba walitawala kwa asilimia kubwa zaidi ya wapinzani wao na kuwapa wakati mgumu kufika langoni, kitu ambacho kilimfanya kipa Ally Salim kutopata kibarua kizito langoni kwake.

 

Mabao ya Simba yamefungwa na Adam Salamba aliyetikisha kamba za Wasomali mara mbili, huku Marcel Kaheza na Rashid Juma wakifunga bao moja moja.

 

Kikosi cha Simba kimecheza bila wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kutokana na kupewa mapumziko, wakati huo nyota Meddie Kagere aliyekuwa anasubiriwa kwa hamu na wanasimba wengi akikosekana japo imeelezwa amerejea Kenya kwa muda.

Mchezo mwingine utakaopigwa saa 10 ni AS Ports ya Djibout itakuwa inacheza na Lydia Ludic kutoka Burundi.