
MIONGONI mwa wanamuziki wanaofanya vizuri kwenye gemu la Muziki wa Hip Hip, Bongo ni William Lymo ‘Bill Nas’, ambaye kwa sasa anatamba na Wimbo wa Tagi Ubavu.
Mbali na kusikika kwa ngoma kali, Bill Bas anatengeneza sana vichwa vya habari kwa stori tofautitofauti.
Over Ze Weekend, limembamba na kupiga naye stori kadhaa, Huyu hapa;
Over Ze Weekend: Vipi kaka mbona kimya sana?
Billnas: Nipo tu muda mwingi sana siku hizi nakuwa studio hivyo nikiwa na kazi mpya napenda sana kutulia.
Over Ze Weekend: Nilijua ndiyo yale mambo ya kwenye mtandao umeamua kujificha.
Billnas: Hapana, mbona kipindi kilekile tu nilianza kutembea.
Over Ze Weekend: Lakini ilikuletea shida gani?
Billnas: Unajua mimi sipendi kuongelea hilo maana lilishapita.
Over Ze Weekend: Sawa, lakini vipi kwa sasa uhusiano wako na Nandy?
Billnas: Tuko vizuri kama kawaida na tunahes-himiana.
Over Ze Weekend: Vipi kwa mpenzi wako zile video hazijakuharibia na kwa ndugu pia?
Billnas: Hapana tuko sawa kabisa na ni muelewa na hata ndugu zangu walikuwa pamoja na mimi kama kawaida.
Over Ze Weekend: Huyo mpenzi wako mpaka sasa bado upo naye?
Billnas: Niko naye na ndiyo natarajia kufunga naye ndoa mwakani.
Over Ze Weekend: Wanamuziki wengi wanaogopa sana kuoa wanajua ndio mwisho wa muziki wao unazungumziaje hilo?
Billinas: Kwangu mimi sidhani kama ipo hivyo, kwa sababu hilo jambo ni wajibu na mimi lazima nilitimize hilo.
Over Ze Weekend: Mwanamke wako ambaye unatarajia kumuoa ni staa?
Billnas: Hapana ni wa kawaida tu ila ni mwanamke anayejiheshimu.
Over Ze Weekend: Vipi kuhusu mipango yako ya baadaye kwenye muziki?
Billnas : Baada ya miaka mitano nataka kuachana na muziki na kufanya biashara tu na muziki utabaki kuwa kwenye damu maana nina ndoto kubwa kwenye maisha yangu.
Over Ze Weekend: Wewe ni rafiki mkubwa sana wa Darasa lakini sasa hivi haonekani kabisa hivyo mashabiki wanataka kujua yupo au amepotelea wapi?
Billnas: Darasa yupo anaendelea na ishu zake za muziki kama kawaida na muda si mrefu watamsikia tu anarudi upya.
Over Ze Weekend: Kuna picha nyingi unaonekana umepiga na mtoto wa Madee, vipi kuhusu na wewe hujabahatika kupata mtoto wa ujanani?
Billnas: Bado ila nitapa mtoto na huyo mke wangu mtarajiwa.
Over Ze Weekend: Haya asante sana.
Billnas: Shukurani.
IMELDA MTEMA