Mawaziri hao walioteuliwa ambapo wengine walikuwa mawaziri isipokuwa wamebadilishiwa Wizara ni pamoja na Kangi Lugola, aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) sasa anakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo amechukua nafasi ya Mwigulu Nchemba.
Musa Ramadhani Sima amekuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Omary Mgumba anakuwa Naibu Waziri wa Kilimo. Prof. Makame Mbarawa aliyekuwa Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anakuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
Mhandisi Isack Kamwelwe anakuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Athumani Kihami ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Na Edwin Lindege | Global Publishers.