




MSANII wa Bongo Fleva ambaye pia ni meneja wa baadhi ya wasanii, Quick Rocka, usiku wa Julai 01, 2018, amefanya ‘Switch Party’ ya kusherehekea pamoja na wasanii wake mafanikio waliyopata.
Pati hiyo imefanyika katika ukumbi wa Life Club na kuhudhuriwa na wasanii kibao walio kwenye lebo ya Switch Record akiwemo Mimi Mars, Whozu na wengine.
Mmoja kati ya mastaa waliofika katika pati hiyo ni Gigy Money aliyeiambia Global TV Online kwamba ugomvi wake na mzazi mwenziye ambaye ni mtangazaji wa kituo cha runinga cha MO J umekwisha na yote aliyoyaongea yalikuwa ni hasira tu bali anampenda mwanamme huyo.