×

Msajili Vyama Aliyesimamishwa na Mwigulu Arudishwa Kazini

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akisalimiana na Msajili wa Vyama wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Merlin Komba (kulia) alipowasili katika ofisi hizo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kukabidhiwa rasmi ofisi baada ya kuapishwa jana. Picha na Ericky Boniphace.

 

MSAJILI wa Taasisi za Kiraia na Vyama vya Hiari wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Merlin Komba, ambaye alisimamishwa kazi na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba,  wiki chache zilizopita kufuatia msajili huyo kuandika barua kwa kanisa la KKKT kutaka lifute waraka wake wa Pasaka, amerudishwa kazini.

 

Siku moja tu baada ya Lugola kuapishwa, Komba amerudishwa kazini. Hata hivyo Lugola amekataa kusema ni nani aliyemrudisha kazini msajili huyo, na kwa utaratibu gani.

 

Mwigulu alisema barua hiyo kwenda KKKT iliandikwa na ‘wahuni’ waliokuwa na lengo la kuhatarisha amani ya nchi.

 

Source Malisa GJ.