×

MASTAA HAWA… NDOA ZIMEWAPITIA KUSHOTO

Ndumbagwe Misayo ‘THEA’

NDOA ni kitu chema na kila mwanamke anatamani kuingia kwenye ndoa. Lakini wapo wanawake ambao wanaingia na kushindwa kuhimili changamoto zake na kuamua kuachika kirahisi.

Kundi lingine ni la wanawake ambao huuingia mkenge wa: “huyu mchumba wangu” na kujikuta wakizawadiwa watoto tu bila ndoa.

Kila mtu ana mipangilio ya maisha yake inawezekana aliyezalishwa bila ndoa aliamua hivyo au alidanganywa na mwanaume kwamba atamuoa lakini ahadi hiyo ikaishia hewani huku wanawake wengine wakiwa hawatamani hata kusikia ndoa kutokana na kutendwa sana na wanaume katika uhusiano wa kimapenzi.

Hata kwenye ulimwengu wa mastaa hapa Bongo hilo lipo ambapo leo katika makala haya tunakuletea orodha kwa ufupi ya mastaa wa kike ambao ndoa zimewapitia kushoto yaani wapo ambao wameolewa na wameachika huku wengine wakiwa hawajaolewa lakini wamezalishwa.

NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’

Mwanamama huyu kabla hajaingia kwenye ndoa alizalishwa mtoto mmoja na mwanaume mwingine, baadaye

MAKALA

akaingia kwenye ndoa na msanii mwenzake, Michael Sangu ‘Mike’ kilichotokea ni kama mlivyosikia. Katika ndoa hiyo Thea alijaliwa kupata mtoto mwingine mmoja lakini akawa bahati mbaya (akafariki) na baada ya hapo hakupata mwingine mpaka walipoachana na kubaki na kumbukumbu ya kuzalishwa nje ya ndoa.Related image

HALIMA YAHAYA ‘DAVINA’

Mama huyu wa watoto watatu alizalishwa watoto wawili na mwanaume tofauti na aliyekuja kuingia naye kwenye ndoa.

Alipoolewa na Abdallah Shakoor alifanikiwa kupata mtoto mwingine mmoja na kutimiza idadi ya watoto watatu, lakini mkeka wa ndoa alishaukunja kitambo.

KAJALA MASANJA

Awali ‘alifyatua’ mtoto mmoja wa kike na prodyuza maarufu nchini, P-Funk, baadaye akajimuvuzisha kwenye kwenye ndoa.

Mwanamama huyu alidumu kwa kipindi kifupi tu; yeye na mumewe wakapata tatizo la kisheria wakaswekwa gerezani. Baadaye Kajala akaachiwa, lakini mumewe akabaki lupango. Hata hivyo, mume naye alipoachiwa akasema: “Mimi tena ndoa, nimekoma.” Akajiweka kando na Kajala na kuamua kuendesha maisha yake mpaka sana.

JENNIFER KYAKA ‘ODAMA’

Huyu hakuwahi kuingia kwenye ndoa lakini amezalishwa mtoto mmoja ambaye hapendi na hakuwahi kumwanika baba wa mtoto huyo hivyo mpaka sasa yupoyupo tu. Ukimwangalia ni msichana wa sura nzuri lakini nini kinachomfanya asiolewe, pengine mjuzi ni yeye.

Related image

YVONNE CHERRY ‘MONALISA’

Mkongwe huyu wa filamu ana watoto watatu kila mmoja na baba yake. Monalisa aliwahi kuolewa na aliyekuwa prodyuza maarufu wa filamu, marehemu George Tyson ndoa ikavunjika wakiwa na mtoto mmoja. Alipotoka hapo akaolewa tena na mwanaume mwingine, akapata naye mtoto mmoja. Mtoto wa tatu alimpata hivi karibuni na hakuwahi kumwanika baba wa mtoto.

JACQUELINE PENTEZEL ‘JACK CHUZ’

Huyu kabla ya kuingia kwenye ndoa alikuwa na mtoto mmoja ambaye alizaa na mwanaume mwingine ndipo akaolewa na Gardner Dibibi lakini ndoa hiyo haikudumu ikavunjika bila kujaliwa mtoto. Dibibi tayari alishaoa mwanamke mwingine huku Jack akiwa bado hajaolewa tena mpaka sasa.

JUDITH WAMBURA ‘LADY JAY DEE’

Mwanamuziki huyu wa Bongo Fleva alibahatika kuingia kwenye ndoa na mtangazaji Gardner Habash lakini ilivunjika na sasa kila mtu na maisha yake. Gardner ana mtoto mmoja aliyezaa na mwanamke mwingine lakini Jide Mungu hajamfungulia bahati hiyo mpaka sasa.

Na Mwandishi Wetu