
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ametoa agizo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumshusha cheo Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, Leopold Fungu.

Lugola ametoa agizo hilo leo Julai 6 wakati akifanya cha kimkakati cha viongozi wa vyombo na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo, ambapo ameagiza RTO Fungu ashushwe cheo hadi kubaki na nyota tatu.
Aidha, Lugola ameagiza Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo.