×

Mbunge Mabula Atembelea Ofisi za Global, Mwanza – Video

Mbunge wa Nyamagana, Stanislaus Mabula leo Jumatatu, Julai 16, 2018 amefanya ziara katika Ofisi za Kampuni ya Global Publishers zilizopo jijini Mwanza na kuzungumza machache na wafanyakazi wa Kampuni hiyo. Pichani ni Mabula (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya waandishi wa Global Publishers, Mwanza.

 

Katika mazungumzo yake, Mabula alizungumzia kuhusu mambo aliyoyafanya kwa kipindi chake cha uongozi kwenye jimbo hilo, tangu alipochaguliwa mwishoni mwa mwaka 2015 na mikakati yake kuelekea mwaka 2020.

VIDEO: MSIKIE MABULA AKIFUNGUKA