×

Kassim Mganga Amrudisha Keisha

MKONGWE kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Khadija Shabani Taya maarufu kwa jina la Keisha, amefunguka kuwa amerudi upya kwenye gemu kwa msaada wa mwanamuziki mwenziye, Kassim Mganga.

 

Akichezesha taya na Mikito Nusunusu, Keisha alisema amekaa kimya bila kutoa ngoma yoyote kwa takribani miaka minne na Kassim ndiye aliyemuandikia wimbo wake mpya uitwao Nioe na anaamini ujio huo utamrudisha Keisha yule aliyesumbua na ngoma nyingi kwenye chati ya muziki Bongo.

“Nimerudi kwenye gemu ninaamini ujio wangu huu mpya utanifikisha mbali na baada ya kutoka audio nitafanya video hivi karibuni,” alisema Keisha ambaye ni mwanasiasa pia kwani ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi.

 

STORI: BONIPHACE NGUMIJE