
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imekubaliana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi ili kubaini kilichotokea kwenye kikosi cha doria cha mbwa na farasi ili kupata ufumbuzi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, alipozungumza na vyombo vya habari kuhusu mikakati ya wizara yake ambapo alibainisha kwamba amefikia makubaliano hayo na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, kuhusu kupotea kwa mbwa mmoja wa doria ambaye bado hajulikani alipo.
“Nilibaini mapungufu pale bandarini wakati wa makabidhiano ya vitabu vya doria vya mbwa hao; wametoka mbwa sita lakini kwenye makabidhiano wanarudi watano,” alisema na kusema jambo hilo liko kwenye uchunguzi.
Na Edwin Lindege | Global Publishers