×

Harmonize Awafungukia ‘Mapacha Wake’, Harmorapa & Harmo Junior

MSANII wa Biongo Fleva kutoka Wasafi ‘WCB’, Harmonize ameibuka na kuwapost Harmorapa na Harmo Junior ambao wanafanana naye kwa sura na muonekano.

 

Harmonize amefunguka na kubainisha namna jina lake linavyoweza kuwanufaisha vijana hasa kwenye tasnia anayoifanyia kazi namaanisha muziki.

 

ALICHOKIANDIKA Harmonize;

“Mwiko kukata Tamaa ama kukatishwa na mtu yeyote yule katika safari yako ya mafanikio hii safari ni ndefu sana….!!! Utakutana na changamoto nyingi mno….!!! yakiwemo matusi, dharau, uonevu, chuki, namengine kibao ila pale utakapokubali kukata tamaa ama kukatishwa utakuwa umewavunja moyo watu wengi sana….!!!!

(1)Familia yako

(2)Ndugu jamaa na marafiki

( 3)Hata wale wachache waliokuwa wanakutia Moyo na motisha uongeze jitihada nawengine wengi mno….!!!

Itakuwa umewavunja moyo …!!

lakini pia M/mungu ni waajabu na hajawahi kukosea katika hii Dunia kila alifanyalo lina maana. Kubwa sana..!!! Wenda kawaumbe Binadam wengine kwa mfano wako nikiwa namaana mnafanana ambalo ni jambo la heri na baraka 🙏

so ukikata tamaa nao pia utakuwa umewaangusha jitihadazako, maarifa, kuzishinda changamoto ndio njia peke inaweza kuleta faraja kwa wengi wanao kuzunguka zingatia hili 👉 #MaishaNiKombolela….!!! God bless my twins brothers 🙏🙏