×

RAIS WA TBF AKABIDHI BENDERA TIMU YA KIKAPU

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu, Phares Magessa (katikati) akimkabidhi bendela nahodha wa timu hiyo.
Zoezi likiendelea.

 

 

Timu  ya Mpira wa Kikapu ya Wazalendo inatarajiwa kuondoka nchini kesho Ijumaa  kuelekea Madagascar kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya 3×3 Africa Basketball Qualifiers ambayo yatashirikisha nchi 16 ikiwemo Tanzania.

 

Katika mashindano hayo timu nne kati ya hizo zitapata nafasi ya kushiriki Fainali za Africa, Afrobasket 3×3  zitakazofanyika nchini Togo, mwezi Oktoba, mwaka huu.

 

Katika timu hiyo ya Tanzania inashirikisha wachezaji walioshiriki mashindano ya 3×3 FIBA Zone V U18 yaliyofanyika hapa nchini na Tanzania kushika  nafasi ya pili na kuingia mashindano ya Afro Basket U18 yatakayofanyika nchini Mali, baadaye mwaka huu.

 

Wachezaji watakaoenda na timu ya Wazalendo ni;

 

1. ABBA PATRICK ROBERT 

2. HAJI RASHID MBEGU 

3. CHARLES ALBERT MAYOMBO  

4. RASHID TARIQ HAROUN MAARIFA 

5. JOVIN CHARLES NGOWE  

6. MWALIMU HERI KIJOGOO  

7. BARAKA NSAJI 

8. PHINIAS STEPHEN KASHABI 

9. JONAS MUSHI

Viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni

1. KARABANI LAWRENCE KARABANI- Meneja wa timu na Mkuu wa Msafara

2. ROBERT MNENDE MANYERERE – Kocha

3. SHABANI MAHOBONYA – Afisa