
Mtoto Ibrahimu Mwenye Kipaji cha kuhubiri na kuombea watu wenye matatizo mbali mbali ameanza kupokea pesa kutoka katika sehemu mbalimbali za dunia ili kumwezesha kununua vifaa vya kuifanya hHuduma yake vizuri zaidi.
Akizungumza na Global TV Online ambayo ilimuibua mtoto huyo, mama mzazi wa Ibrahim amesema amepokea michango na simu nyingi za pongezi kwa mwanaye kutoka kwa watu wa Marekani, Mwanza, Kwa Mromboo na sehemu zingine nchini Tanzania.
Mama Ibra amesema wengi wao wameonyesha kuguswa na kiupaji cha kutoa huduma ya maombezi na uponyaji inayotolewa na mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9.