×

MBWA HAJAPOTEA ILA ALIKUWA MAFUNZONI

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakaluka.

MSEMAJI wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakaluka amesema mbwa anayedaiwa kupotea hakuwa amepotea bali alikuwa  katika mafunzo.

 

Amesema mbwa huyo alikuwa katika bwalo akiendelea na mafunzo na hivyo amewaomba Watanzania kufahamu hakuna mbwa aliyepotea.

 

Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam Mwakaluka amefafanua mbwa anayedaiwa kupotea yupo kwenye mikono salama ya Jeshi la Polisi na kwamba yupo kwenye mafunzo.

 

Amefafanua kuwa wakati wa  ziara ya Waziri wa Mambo Ndani alipokwenda bandarini hakumkuta mbwa hiyo hivyo baadhi ya waandishi wakadhano amepotea lakini ukweli ni kwamba alikuwa mafunzoni.

 

“Mbwa yupo kwenye mikono salama na yupo kwenye mafunzo,habari ya kwamba mbwa ameonekana Kenya si kweli,”  amefafanua.Alipoulizwa mbwa huyo alikuwa katika mafunzo ya aina
gani,Mwakaluka amejibu hawezo kuelezea aina ya mafunzo ambayo amepewa  kwani hayo ni mambo ya kitaaluma na ni kwa ajili ya Polisi.

 

Kuhusu cheo cha mbwa huyo amesema hana cheo bali ni mbwa mwenye mafunzo ya
polisi na wameamua kutoa ufafanuzi huo ili umma ujue kuwa mbwa yupo na
wala hajapotea.