×

Kigoma: Wasiojulikana Wavamia Zahanati, Waiba Dawa

WATU wanaosaidikiwa kuwa ni majambazi, wamevamia zahanati ya Kijiji cha Nyumbigwa wilayani Kasulu mkoani Kigoma na kuiba dawa katika chumba cha kuhifadhia dawa ikiwa ni mwendelezo wa kuwepo kwa matukio ya kuvamia na kupora dawa katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za afya wilayani humo.

 

Akitoa taarifa ya wizi huo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Moshi Kigwinya,  amesema miongoni mwa dawa zilizoibwa ni zile zisizouzwa na serikali ambazo zina zaidi ya thamani ya shilingi milioni nne.

 

Kamanda wa Polisi wilaya ya Kasulu, Maisha Maganga,  amesema tayari jeshi la polisi limeanza uchunguzi huku akitoa wito kwa viongozi wa vijiji kuacha kuajiri walinzi wachache ambao, hata hivyo, wengi wao ni wazee ambao hawana uwezo wa kukabiliana na matukio ya uhalifu.