
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam, Mwita Mwikabe Waitara aliyetangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kuhama kutoka CHADEMA kwenda CCM, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea tena Ubunge katika jimbo hilo alilokuwa akiliongoza.
Waitara alitangaza kuhama CHADEMA kwa kile alichodai kuwa haridhishwi na mwenendo wa demokrasia ndani ya chama hicho, Freeman Mbowe kung’ang’ania madaraka ya Uenyekiti wa chama hicho taifa, pamoja na matumizi mabaya ya ruzuku.