MAJALIWA APOKEA MIFUKO 50 YA SARUJI KWA AJILI YA JIMBO LA BUKENE
Global Publishers August 17, 2018
SHARE THIS:
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemkakabidhi mbunge wa Bukene, Selemani Zedi mifuko 50 ya saruji iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora kupitia CCM, Munde Tambwe baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa wa Bukene wilayani Nzega Agosti 17, 2018.
Saruji hiyo imetolewa kwa jimbo la Bukene ili isaidie katika ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii jimboni humo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ameshuhudia tukio hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi mbunge wa Bukene, Selemani Zedi (kushoto) mifuko 50 ya saruji iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora kupitia CCM, Munde Tambwe (wapili kushoto ) baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa wa Bukene wilayani Nzega Agosti 17, 2018 saruji hiyo imetolewa kwa jimbo la Bukene ili isaidie katika ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii jimboni humo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Taifa wa Bukene wilayani Nzega, Agosti 17, 2018.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia saruji iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora kupitia CCM, Munde Tambwe.