
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa sugu 13 kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya jiji na mikoa ya jirani.
Watuhumiwa hao ni BALIZANILA EZEKIEL (37) Raia wa Burundi, SHUKURU HASSAN (38), SAIDI SHABANI (34) HAJI SALUM (38) FRENK KALIKENE (32) na wengine 8.
Watuhumiwa hao wamekuwa wakiendelea na vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha licha ya kuachiwa huru baada ya kumaliza vifungo vyao katika magereza mbalimbali hapa nchini.

Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na bostola aina ya Chinese star iliyokuwa na risasi nne ndani ya magazine, pamoja na risasi nyingine tisa zikiwa zimehifadhiwa pembeni.
Oparesheni hii ni endelevu ya kupambana na wahalifu wote wanaofanya unyang’anyi ndani ya jiji la Dar es salaam na wanaokuja kujificha jijini Dar es salaam baada ya kufanya uhalifu kutoka mikoa ya jirani.
KUKAMATWA KWA MTANDAO WA WIZI WA PIKIPIKI
Mnamo tarehe 26 Julai 2018 majira ya 18:00 hrs huko maeneo ya Tandika Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu(3) kwa tuhuma za uporaji wa pikipiki kisha kuziuza mikoa ya jirani.
Watuhumiwa hao ni NASSORO RAJABU KAFYA (23) mkazi wa Lumo, SALUMU MKWAVILA (23) mkazi wa Tandika Manguruwe na SAID KHAMIS LIKOKA (27) mkazi wa Mbagala Saku, katika mahojiano watuhumiwa walikiri kufanya uhalifu huo na kuwataja washirika wenzao wawili ambao hutengeneza kadi na plate namba bandia ili waweze kuziuza pikipiki hizo.
Askari walifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kuwakamata wafanyakazi wanne kutoka kampuni zilizopewa zabuni ya kutengeneza plate namba za magari na pikipiki nchini; kampuni ya Masasi Sign na Autozone Ltd ambao ni PRISCA HOSEA (32), EDNA STEVEN (31), ALLY MOHAMED (34), na ARAFA HAMID (38). Ambao wamekuwa wakighushi kadi na plate namba za pikipiki hizo kabla ya kuuzwa.
Operesheni ya kali inaendelea ili kutokomeza mtandao wote wa uporaji pikipiki, kutengeneza kadi bandia na plate namba ambazo hubandikwa kwenye pikipiki na kisha kuuzwa.
opAresheni dhidi ya wahujumu miundombinu ya mashirika ya SERIKALI NA kampuni za simu.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na Tanesco, Dawasco na kampuni mbalimbali za simu za mkononi kuanzia tarehe 27 Agosti 2018 litafanya operesheni kali dhidi ya watu wanaohujumu miundombinu ya mashirika hayo.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la watu kujiunganishia maji safi kutoka kwenye mabomba ya DAWASCO bila kufuata utaratibu, pia wanaojiunganishia umeme kinyume na utaratibu, kuiba mafuta ya transformer na kuiba betri kwenye minara ya kampuni za simu hapa jijini Dsm.
Aidha Jeshi la Polisi kuanzia sasa linawataka watu wote wanaojihusisha na uhalifu huo kuacha mara moja na kujisalimisha wenyewe katika vituo vya Polisi au katika mashirika na kampuni hizo kabla ya kuanza kwa oparesheni hiyo kali, na watakao kaidi agizo hili watakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.
(PICHA/HABARI: DENIS MTIMA -GPL)