
POLISI mkoani Kilimanjaro inawashikilia watu wawili wakazi wa mjini Moshi kwa tuhuma za kukutwa na gari la wizi linayosadikiwa kumilikiwa na Ikulu ya Nairobi nchini Kenya ambalo liliripotiwa kuibiwa Agosti 19 mwaka huu.
Gari hilo aina ya Nissan Patroll V8 Black lenye namba za usajili KCP 184 RV lakini likiwa limebandikwa namba bandia ambazo ni T 954 DEQ, limekamatwa kwenye kizuizi cha Msomali mjini Bomang’ombe wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Kilimanjaro, gari hilo lilikamatwa likiwa njiani kuelekea Kilimanjaro likitokea Kenya na baada ya kuwahoji watuhumiwa hao walitoa nyaraka zinazotofautiana na wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
CREDIT: Azam TV