×

JUX AMUWEKA PEMBENI VANESSA, AJA KIVYAKE

MSANII wa muziki wa ki­zazi kipya, Juma Mussa ‘Jux’, ametamka kuwa kwa sasa anaweka pembeni ziara yake na msanii mwenzake, Vanessa Mdee ‘V Money’ ya In Love With Money kisha kuelekeza nguvu katika kutengen­eza video na nyimbo.

Jux amekuwa akifanya ‘tour’ hiyo ya In Love With Money pamo­ja na V Money ambaye pia ni mpenzi wake ambapo wawili hao wamezunguka mikoa mbalim­bali kwa ajili ya tour hiyo.

Akizungumza na Kilinge, Jux anayetamba na ngoma kibao zikiwemo Looking For You, amesema kwa sasa anadili zaidi na kuten­geneza nyimbo zake yeye kama yeye na kuweka pembeni kwa muda suala la tour yao hiyo.

“Kwa sasa ninataka kuja na pro­jekti zangu mimi kama mimi na siyo tena na Vanessa kama ambavyo tume­kuwa tukifanya kwenye hii tour ya In Love With Money, nina­chofanya ni kutengeneza video na nyimbo zangu.

“Unajua hiyo tour haijafika mwisho, tutaendelea kuifanya ila kwa sasa ninafanya mambo yangu kama mimi kisha baadaye tena tu­tarudia kuzunguka mikoa mbalimbali,” alisem a Jux.

Said Ally, Dar es Salaam.