
Msanii wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu leo amefunga pingu za maisha na aliyekuwa mpenzi wake Upendo Meja katika Kanisa la AKUZAMU lililopo Kinondoni Biafra Jijini Dar.
Katika ndoa hiyo vifijo na nderemo vililindioma kanisani hapo haswa wakati wawili hao wakilishana viapo na baada ya kutangazwa kuwa wawili hao ni mke na mume.

Ndoa hiyo ilionekana kuwa ya furaha kufuatia maharusi hao wageni waalikwa pamoja na waumini wa kanisa hilo kuserebuka sebene la nguvu lililokuwa likiporomoshwa na bendi ya kanisa hilo.





PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL