×

SERENGETI BOYS YAMALIZA NAFASI YA TATU CECAFA, WANYAKUA TUZO

TIMU ya Taifa ya Viajana ya Tanzania walio chini ya Umri wa Miaka 17 (U17), Serengti Boys imemaliza mashindano ya CECAFA kwa ushindi wa mabao 4-3 kwa njia ya matuta dhidi ya Rwanda baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

 

Serengeti imemaliza hatua hiyo baada ya kutolewa na Uganda ambayo ipo dimbani hivi sasa kucheza na Ethiopia kwenye mchezo wa fainali, mabao 3-1. Mechi ya fainali kati Uganda na Ethiopia imehudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Ahmad Ahmad.

 

Aidha, Tanzania imepewa Tuzo ya Timu yenye nidhamu kupitia Serengeti Boys Katika mashindano hayo huku Mchezaji wa Serengeti Boys, Kelvin John akichaguliwa kuwa mchezaji Bora wa michuano ya Cecafa Total U17 Afcon Zonal Qualifiers.