×

MAHAKAMA TANGA YAWATUNUKU VIONGOZI  WALIOSTAAFU

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akizungumza jambo katika haflla hiyo, wa pili  kushoto ni Mhe. Jaji Imani Aboud na kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi Kanda ya Tanga, Mhe. E.J. Mkasimongwa.
Viongozi mbalimbali wa Serikali waliohuhuria.
Baadhi ya watumishi waastafu walioagwa kwenye hafla hiyo kushoto ni Bi. Bi. Lydia Yohana Andrew  na kulia ni Bi. Shehu Ally Muhsin.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni, Mhe. Arnold Kileo, akipokea cheti kwa kushika nafasi ya kwanza kwa Mahakimu wa Wilaya waliosikiliza na kumaliza mashauri mengi.
 Afisa Tawala Mahakama ya Wilaya ya Korogwe, Emmanuel Machimo, akipokea cheti kwa kushika nafasi ya kwanza kwa kada ya Maafisa Tawala, Utumishi Kanda ya Tanga.
Mhasibu Msaidizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Bi. Elizabeth Noah Mavoa, akipokea cheti kwa kushika nafasi ya pili ya Mhasibu bora Kanda ya Tanga.
Bi. Shehu Ally Muhsin  akipokea zawadi.

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Tanga imewapongeza baadhi ya Watumishi wake waliofanya vizuri kwa kuwapa vyeti maalum ikiwa ni ishara ya kutambua mchango pamoja na juhudi zao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

 

 

Vyeti hivyo vilitolewa kwa watumishi hao na mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bw. Martine Shigela, Agosti 24, 2018 katika hafla fupi ya kuwaaga  Majaji na Mahakimu waliohamishwa vituo pamoja na watumishi wa kada mbalimbali waliostaafu.

 

 

Utaratibu huu umeanzishwa katika kanda hii ili kuenzi jitidaha na ufanisi wa kazi waliokuwa nao kipindi cha utumishi wao.

 

 

Miongoni mwa Watumishi waliopatiwa vyeti hivyo ni pamoja na Mahakimu wa Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo, Maafisa Utumishi, Wasaidizi wa Kumbumbuku, Wahasibu, Makatibu Mahsusi, Madereva, Walinzi, Mahakama za Wilaya zilizofanya ukarabati mkubwa wa Mahakama za Mwanzo, Kituo kilichoongoza kwa watumishi wake kuvaa sare na kuonekana nadhifu pamoja na Mahakama za Wilaya na Mwanzo zilizosikiliza na kuamua mashauri kwa asilimia nyingi kuliko zingine.

 

 

Watumishi waliostaafu ambao waliagwa katika hafla hiyo ni Bwana. Jumbe Athumani Kai, Msaidizi wa hesabu, Mahakama ya Wilaya Korogwe, Bi. Lydia Yohana Andrew Msaidizi wa kumbukumbu, Mahakama ya mwanzo Mashewa Wilayani Korogwe na Bi. Shehu Ally Muhsin, Msaidizi wa kumbukumbu Mahakama ya Wilaya ya Tanga.

 

 

Viongozi wengine waliohudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na Mkuu wa chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto IJA, Mhe Jaji Faustine Kihwelo, Mkuu wa Wilaya wa Handeni, Mhe. Godwin Gondwe, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Mhe. Sauda Mtondoo, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Thobias Mwilapwa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji – Korogwe, Nicodemus John, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto  na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba.

 

Na Amina Ahmad, Mahakama Kuu-Tanga