×

TIC: TAASISI ZITUSHIRIKISHE KUTATUA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji (TIC), Geofrey Mwambe,  akizungumza na waandishi wa habari.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.

 

MKURUGENZI  Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Geoffrey Mwambe,  amewaomba viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali, sekta binafsi na wananchi kwa jumla kukishirikisha kituo cha uwekezaji Tanzania pale wanapokuwa wakishughulikia changamoto mbalimbali zinazohusiana na uwekezaji ili kituo hicho kiweze kushauri njia bora za kushughulikia changamoto zinazoweza kujitokeza.

 

Mwambe amesema hivyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya ziara yake ya kikazi nchini Korea Kusini na China iliyolenga kuwahamasisha na kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta ya afya hususani sekta ya viwanda vya kutengeneza madawa na vifaa tiba.

 

“Kituo kinawahamasisha wajasiriamali waweze kuzalisha bidhaa zao wakilenga katika upatikanaji wa malighafi za kulisha viwanda wakati tunapoelekea katika kujenga uchumi wa viwanda,” alisema Mwambe.