
MWANADADA Faidha Omari ‘Sister Fay’, ambaye kwa sasa anatengeneza vichwa vya habari kutokana na uhusiano na ‘benten’ wake aitwaye Hollystar, amewatolea uvivu watu wote wanaomdisi kisa mpenzi wake huyo kwamba anambemenda, wanamuonea wivu na wanataka kumpora mpenzi wake huyo.
Akichonga kiaina na Star Showbiz, Sister Fay’ alisema kuwa, katika ulimwengu wa sasa suala la umri ni namba na halina tatizo kwenye uhusiano na kwamba amewashitukia wote wanaomsemasema kuwa kunakitu wanakitaka kwa mpenzi wake huyo.
“Wanaonisema mara sijui ninambemenda mpenzi wangu wanataka kunipora na hakuna lolote, kwani simbemendi na mimi nina uhakika tunaendana,” alisema Sister Fay.