






Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe leo ametembelea Kampuni ya Global Group ambayo ndani yake kuna Global TV Online ambapo alipata fursa ya kutembelea studio zza Global TV.
katika ziara hiyo Waziri Mwakyembe ampata maelezo ya namna ambavyo Global Tv Online inavyoweza kutumia teknolojia ya Kubalisha Background ya kijani na matumizi ya Vitual Studio katika kurusha matangazo yake.
Mkuu wa Idara ya Global Tv James Range amemuelezea Waziri Mwakyembe kuwa kwa kutumia Green Screen Technology wanaweza kubadili muonekano wa studio na kuwa wa kisasa zaidi kadiri ya mahitaji ya vipindi husika.
Akiwa katika Studio za Global Tv, Waziri Mwakyembe ameweza kufanyiwa mahojiano maalumu na Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli ambapo Mh Waziri amepata fursa ya kufafanua masuala kadhaa ya kitaifa