
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako amefungukia sakata la mtoto wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kibeta, Sperius Eradius (13) aliyefariki duniakwa kupigwa bakora na mwalimu wake kwa kutuhumiwa kuiba pochi ya mwalimu wilayani Bukoba, mkoani Kagera juzi, Jumatatu, Agosti 27, 2018.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam, Prof. Ndalichako amesema mwalimualiyefanya hayo hakutumwa na serikali, hivyo wananchi wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu na waviachie vyombo vya dola vimshughulikie kwa mujibu wa sheria.
Edwin Lindege | Global Publishers.