
Katika jitihada za kujiimarisha na kuboresha huduma zake, hoteli yenye hadhi ya Nyota Tano (Five Star Hotel), Hyatt Regency ya jijini Dar es Salaam, imekuja na habari njema kwa kuzindua vyumba vipya vizuri kwa bei ya wastani ili kuwawezesha wageni na wenyeji kupata huduma ya malazi na chakula kwa gharama nafuu.

Uongozi wa hoteli hiyo maarufu na kongwe nchini Tanzania, ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kwa jina la The Kilimanjaro Hotel, umefanya mabadiliko makubwa na kuendelea kutoa huduma za kiwango cha kimataifa, tangu ilipoanza kufanya shughuli zake chini ya jina la Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.

Global Publishers ni miongoni mwa wadau walioonja ubora wa huduma na uzuri wa vyumba hivyo wikiendi hii ambapo ilijionea mandhari nzuri na ya kuvutia katika vyumba hivyo vipya baada ya kukaa na kulala kwa siku moja katika hoteli hiyo inayotazama Bahari ya Hindi.

Kwa maelezo zaidi ya namna ya kufanya ‘booking’ na kujua gharama zao, tafadhali watembelee kwenye mitandao yao ya kijamii ya FaceBook, Instagram na Twitter kwa jina la; hyatt_kilimanjaro au watembelee kwenye website yao kwa kubonyeza Link =>bit.ly/2wheQci 
