RAPA kijana wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mkosoaji wa Rais Joseph Kabila “amepotea” tangu Jumatano iliyopita.
“Bob Elvis Masudi amepotea tangu Jumatano alipokuwa akienda nyumbani kwa prodyuza kwa ajili ya kuachia albamu yake ya “Anti-mediocrity’”, alisema mtu mmoja aliye karibu na mwanamuziki huyo.
Aliongeza: “Familia haijamwona tangia Jumatano usiku, hapatikana kwenye simu yake, licha ya kwamba ni mpenzi wa mitandao ya kijamii.”
Mkuu wa polisi wa Jiji la Kinshasa, Sylvano Kasongo, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba ameshangazwa na suala hilo akiongeza: “Hakuna mtu wa familia yake ambaye ameripoti kupotea kwake polisi.”