×

BREAKING: Polisi Wafunguka Kuhusu Waliompiga Raia Dar – Video

Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata bastola moja aina ya Browing yenye namba A 183847 ikiwa na risasi tatu ndani ya Magazine, pamoja na silaha nyingine aina ya Shot Gun iliyotengenezwa kienyeji.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema mnamo Agosti 29 mwaka huu, majira ya saa moja usiku, huko maeneo ya Mbagala Kiburugwa

Jeshi la polisi liliwakurupusha wahalifu ambao walikuwa katika mipango ya kutekeleza uhalifu katika maeneo hayo na baada ya kukurupushwa walikutwa wakiwa na mapanga, na baada ya wahalifu hao kuwaona askari waliokuwa katika doria walianza kujihami kwa kuwamiminia polisi risasi, ambapo askari walijibu mapigo na kuwajeruhi wahalifu wawili ambao walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali.

 

Katika hatua nyingine, RPC Mambosasa amezungumzia suala la askari Mgambo waliomshambulia raia kwa kile kinachodaiwa ni kutokana na pesa ya usafi.