×

AKOTHEE ATAMBA KUWA NA ‘MABODIGADI’ 20

 

Esther Akoth ‘Akothee’

KAMA ulikuwa unajua msanii Eric Omondi haishiwi vituko nchini Kenya, basi jua ulikuwa ukijidanganya sana! Taarifa ikufikie kuwa, staa wa muziki nchini humo, Esther Akoth ‘Akothee’ ndiye msanii asiyeishiwa vituko nchini humo ambapo moja ya kituko alichokitoa hivi karibuni ni kujinadi mitandaoni kuwa ana waangalizi wa kumlinda takriban ishirini eti kwa sababu yeye ni maarufu na pia anaendesha gari la thamani.

 

Kama ilivyo kwa mastaa wengi Bongo wanavyoigiza maisha yao kwenye mtandao wa Instagram, Akothee naye alitumia ukurasa huohuo kwa kuposti video akiwa anakula na kusema; “Nimeshakuwa maarufu na umaarufu ni mgumu, kwa sasa siwezi kutoka hovyohovyo kama mwanzo kwa sababu watu wengi sasa hivi wananifuatilia.

 

“Maisha yangu yana drama nyingi sana ila mimi sifeki maisha nina gari kubwa na zuri, nina bodigadi kama ishirini hivi na ninawatumia kwa matumizi yangu mbalimbali pia nina watoto wawili Wazungu, watatu Waafrika ingawa siwashawishi waje kuwa na watoto wengi kama mimi.”