
MBUNGE wa Mikumi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule (Profesa Jay), amefiwa na baba yake mzazi, Mzee haule leo akiwa katika Hospitali ya St. Kizito, Mikumi, ambapo alikuwa asafirishwe kwenda kupata matibabu zaidi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Prof. Jay amethibitisha kifo hicho katika mawasiliano aliyoyafanya kwa njia ya simu akiwa Dodoma.