
MUZIKI ume-kuwa na ladha tofauti-tofauti, achana na ile ‘kubung-kubang’ iliyozo-eleka zamani, kwa sasa miongoni mwa staili zinazo-tamba zaidi ni ‘trap’. Hapa nazun-gumzia kimataifa, na ukitaka kuthibitisha hili tazama wanamuziki wengi duniani kwa sasa wanavyoiga swaga za Kundi la Migos, ambao ni wakali wa ngoma za trap na waanz-ilishi wa stairi ya ‘kudab’.
Sasa ukija Kibongo Bongo ukitaja wanamuzi ambao wanagusagusa kwenye midondoko ya stairi hiyo huwezi kuacha kulitaja jina la Musa Ramadhani ‘Chin Bees’ kutoka lebo ya Wanene Entertainment. Chin Bees ni moja ya alama kubwa ya muziki huo hapa Bongo. Ili ‘kumuinjoi’ tazama ngoma yake ya Kababaye, Pepeta na nyingine nyingi ambazo zinapatikana kwenye albamu yake iitwayo Ladha, ambayo ameiachia mwanzoni mwa mwaka huu.
Hata hivyo, kufanya kwake vizuri kwenye gemu ndiko kumempa mashabiki wengi Afrika Mashariki, na bila shaka kuna mengi ungependa kusikia kutoka kwake, huyu hapa akifanya mahojiano na Ijumaa Showbiz!
Showbiz: Mapema mwaka huu umeachia albamu, kwa sasa wasanii wengi hawafanyi hivyo, wewe nini hasa kilikushawishi?
Chin Bees: Kiukweli kwenye hili sikuamua mwenyewe, nilikaa na menejimenti yangu tukaamua kutoa zawadi kwa mashabiki kama shukurani kutokana na sapoti wanayotupa.
Showbiz: Kwa hiyo huikuwa kibiashara?
Chin Bees: Ndiyo. Sikuuza.
Showbiz: Hakuna hasara uliyopata?
Chin bees: Kwani watu wakipeleka zawadi kijijini kwao kwa ndugu na jamaa huwa wanapata hasara? Ni sawa na nilichofanya, nipo lebo na ninafanya kazi muda wowote kutokana na ratiba.
Lakini imekuwa na faida kwangu kwa sababu watu wamezifahamu nyimbo zangu nyingi na nikiwa kwenye shoo ninaimba nao.
Showbiz: Ukitoa albamu mpya unaweza kutoa bure kama ulivyofanya?
Chin Bees: Nafkiri nikikaa na menejimenti yangu kwenye maandalizi ndiyo nitafahamu nini tutafanya.
Showbiz: Upo kwenye lebo na mwanamuziki Young Killer, kuna changamoto zozote anakupa kwenye kazi?
Chin Bees: Hapana, Young Killer ametoka kabla yangu mimi na mimi nimekuja baadaye kimpango wangu. Kwa hiyo kila mtu anafanya yake, na kila mtu anamuziki wa aina yake.
Showbiz: Ni msanii gani Bongo ambaye unatamani kufanya naye kazi?
Chin Bees: Sijafikiria sana, lakini wanamuziki wakubwa wapo wengi kama Diamond, ambaye ni miongoni mwa wanamuziki ninaowakubali kwani ana swaga za kinyamwezi.
Showbiz: Ilikuwaje ukafanya kolabo na Kaligraph Jones, kwenye remix ya Kababaye?

Chin Bees: Kaligraph aliupenda wimbo maana alipousikia ulimvuruga, akanitafuta na kusema tufanye remix. Kwangu lilikuwa jambo kubwa sana na nilifurahi. Lakini pia nimefuatilia na kugundua kwamba kuna wasanii mpaka Uganda wanatumia melodi zangu na wanasampo nyimbo zangu na wanaziachia huko kwao kama za kwao kabisa.
Showbiz: Upo ndani ya uhusiano?
Chin Bees: Nipo kwenye uchumba. Lakini mtu wangu yupo mbali, so siwezi kuweka zaidi juu ya hili.
Showbiz: Una amini kiki ‘inaboost’ muziki?
Chin Bees: Hapana. Ila upande mwingine ni chaguo la mtu. Kama anayefanya anaona inamsaidia fresh, lakini mimi ninaamini kupitia kazi nzuri.
Showbiz: Unakipi cha kuwashauri wasanii ambao wanatumia dawa za kulevya?
Chin Bees: Siyo mpanga kwa sababu ukitumia dawa inamaanisha una feli, kwa hiyo waachane na hayo mambo.
Showbiz: Kipi unachakumalizia?
Chin Bees: Nina kazi yangu ipo mezani inaitwa Inogile ambayo itatoka hivi karibuni na imepikwa na producer kutoka Marekani ambaye alishawahi kufanya nyimbo zangu mbili ambazo ni Pepeta na Nitulize, mashabiki wangu wawe tayari kwa mzigo huu maana ni hatari sana!