×

OHOOO! MAMA ASAULA UWANJANI

MAMA mmoja ‘jimama’ ambaye inasemekana ni mke wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Latifa, mkazi wa mjini hapa, ametia aibu kubwa baada ya kusaula nguo kwenye Fainali ya Michuano ya Ndondo Cup huku akimwacha mwanaye mchanga akiangua kilio.

 

Tukio hilo lililojiri mwishoni mwa wili iliyopita lilishuhudiwa na gazeti hili na zaidi ya wanaume elfu mbili waliojitokeza kwenye fainali hiyo. Fainali hiyo ilikuwa kati ya timu ya Black Viba na Bajaji FC inayomilikiwa na madereva wa Bajaj mjini hapa ambayo mama huyo ndiyo aliyokuwa akiishabikia.

 

Katika hali ya kushangaza, wakati wa mapunziko, Latifa, akiwa na mtoto aliyekuwa anaangua kilio mgongoni aliwavamia wachezaji wa Bajaj na kuanza kuwafuta jasho kwa kutumia mtandio wake kabla ya kuwapagawisha kwa kuvua nguo katikati ya uwanja.

 

Miongoni mwa wachezaji waliopata ‘huduma’ ya mama huyo ni pamoja na mchezaji wa timu ya Singida United, Miraj Adam Seleman ‘Tata’. Wakati Miraj akicheza fainali hiyo, siku hiyohiyo timu yake ya Singida United ilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida hivyo gazeti hili lililazimika kumuulika kulikoni ambapo alijibu:

 

“Nimezinguana viongozi wangu hivyo nimeamua kurejea hapa nyumbani Moro, mambo yakikaa sawa, nitarejea kwenye timu yangu.” Miraj ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Timu ya Reli ya Moro na Simba ya Dar, Adam Seleman ‘Tata’.

 

Katika tukio hilo, Latifa mwenye mwili mkubwa, bila kujali wingi wa wanaume, wakati huo wa mapunziko alimkabidhi mtoto shoga yake kisha akaingia katikati ya uwanja na kuanza kufanya balaa la kushaula.

 

Mbali na kusaula na kusababisha watu kupiga makelele, Latifa alikuwa akijiviringisha chini huku akijibinua kwa staili za michezo ya chumbani zaidi, mbele ya watoto na mgeni rasmi ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samwel Msuya ambao walimshuhudia mubashara kabla ya kuondolewa uwanjani kupisha kipindi cha pili cha mechi hiyo.

 

Hivi karibuni kumezuka tabia chafu kwenye michuano ya Ndondo ambapo kila timu yenye uwezo kifedha hukodi wanawake kwa sharti la kuwashangilia kwa staili ya kumwaga ‘lazi’. Baadhi ya wanaume waliomshuhudia Latifa uwanjani hapo walilaani vikali kitendo hicho.

STORI: Dunstan Shekidele, Morogoro.