×

JPM: Walisema Mtaka Hafai Kuwa Hata DC, Leo Anaongoza Kuchapa Kazi – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameendelea na ziara yake ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchini ambapo leo Septemba 08, ametembea mkoa mpya wa Simiyu na kufanya mkutano wa hadahara wa kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.

 

Rais Magufli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwaletea maenedeleo wananchi wa mkoa huo;

 

“Wakati nataka kuteua wakuu wa Mikoa, vyombo vyangu viliniambia Mtaka hafai hata kuwa DC, niliamua kumchagua kuwa Mkuu wa Mkoa, baada ya muda nilipoomba ripoti ya utendaji wa wakuu hao wa mikoa, wakasema Mtaka ndiyo namba moja. Unaweza kuona watu wazuri ndiyo huwa wanapigwa vita. Mtaka Chapa kazi!” alisema Magufuli.