×

DRAKE, MEEK MILL WAMALIZA BIFU KATIKA SHOO YA DRAKE

Meek na Drake (kulia).

BIFU kali lililowahi kutokea katika medani ya marapa wa Marekani — kati ya  Drake  na Meek Mill — lilimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita, Jumamosi, katika shoo iliyofanywa n Drake huko Boston.

 

Mwaka 2015 maraPa hao wawili walianza bifu baada ya Meek kusema Drizzy alikuwa anasaidiwa kuandika nyimbo na watu wasiojulikana ambapo Drake naye alitunga nyimbo kum-diss mbaya wake huyo katika albamu ya “Back to Back.”

 

Hata hivyo, baada ya Meek kujikuta jela kutokana na makosa fulani aliyoshitakiwa na baadaye kuachiliwa, alisema bifu lake na Drake lilikuwa limekwisha kwa vile alikuwa iongoni mwa watu waliounga mkono kuachiliwa kwake.