×

Anaswa kwa Kulewesha Wanawake, Kuwabaka na Kulawiti – Video

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kutumia kikosi chake chenye weledi, uadilifu na uwezo mkubwa, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakijihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu, akiwemo njemba mmoja, Kennedy John (35) anayetuhumiwa kuwalewesha na kuwabaka na kuwalawiti wanawake.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP. Jonathan Shanna amesema mwanaume huyo amekuwa akiwalaghai wanawake katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwabaka, kuwaingilia kinyume na maumbile na kuwaibia.

 

Pia jeshi hilo linamshikilia wanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Sonia Fanuel kwa kosa la kujihusisha na wizi wa kutumia funguo bandia (Master Key).

VIDEO: TAZAMA TUKIO HILO HAPA