



VIONGOZI wawakilishi wa vyama vya Madereva kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wamekutana leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanzisha Shirikisho la Vyama vya Madereva Tanzania ambalo litakwenda sambamba na kuwachagua viongozi watakaounda shirikisho hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Abdallah Lubara ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na alikuwa akimaliza mda wake, amesema kuwa shirikisho hilo litakuwa ndiyo kiunganishi cha madereva na wadau mbalimbali katika kuhakikisha fani ya udereva inaheshimika kama fani nyingine.
“Kwa sasa kazi ya udereva inaonekana kama kazi ya mwisho kwa mtu kufikiria kuifanya kwa sababu haina ujuzi, ukitaka leseni tu unaipata hata kiujanjaunjanja. Hii siyo sawa, tunataka kazi ya udereva itambuliwe kama kazi nyingine na yenye kuhitaji vigezo ili kuipata,” alisema Abdallah Lubara.
Ameeleza kwamba, urasimishaji wa shirikisho hilo itasaidia kuhakikisha mchango wa madereva kwenye pato la Taifa unaonekana na kuthaminiwa kutokana na kwamba, kwa sasa madereva wanashindwa hata kuchangia taifa kwa kulipa kodi kwa kutokuwa na mfumo rasmi wa ajira hiyo.
Pia, mkutano huo umewahusisha wajumbe mbalimbali, viongozi wawakilishi wa vyama vya madereva kutoka mikoa ya Tanzania.