×

MKUTANO MKUU WA WAUZA MAGAZETI WAFANYIKA DAR

Baadhi ya wajumbe wa Umoja wa Wauza Magazeti  wakiwa katika mkutano.

MKUTANO Mkuu wa Umoja wa Mawakala Wauza Magazeti umekutana na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu Saccos yao waliyoianzisha miaka mitatatu iliyopita ambayo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda.

Mkutano ukiendelea. 

Umoja huo umekutana leo katika Shule ya Msingi Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo  wamezungumzia juu ya baadhi ya wanachama wa saccos hiyo waliokopa mkopo na hawajarudisha wakitakiwa warudishe fedha hizo ili wanachama wengine wapate kukopa.

Taswira ilivyoonekana ukumbini.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti, Abdurahman Kapaka,  amesema  kikao cha leo kilikuwa ni kujadili mwenendo wa kuboresha Saccos yao na namna ya kuiendeleza kwani baadhi ya wanachama wamefanikiwa kunufaika na Saccos hiyo kutokana na kukopa na hivyo akaomba wanachama ambao hawajarejesha mikopo yao kuirejesha kwa wakati ili kuondokana na usumbufu kwa wengine.

Wajumbe wakisikiliza hoja mbalimbali.
Meza kuu ilivyokuwa.