×

Victoire Ingabire, Kizito Mihigo Waachiliwa Huru Rwanda

Victoire Ingabire.

MWANASIASA  wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire,  ameachiwa huru leo Jumamosi kufuatia baraza la mawaziri nchini humo kuidhinisha amri ya ‘huruma’ ya Rais lilipokutana jana Ijumaa. Ingabire ameachiwa sambamba na wafungwa wengine 2,140.

Mbali na Ingabire ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alifungwa miaka kumi mwaka  2015 kwa kupanga njama za kumuua Rais Paul Kagame.

Mwanamuziki Kizito Mihigo

Kwa mujibu wa shirikala habari la AFP, alipokuwa akitoka jela, Ingabire alimshukuru Kagame akisema huu ndiyo mwanzo wa kufunguka kwa sehemu ya kisiasa nchini Rwanda.

Lakini Waziri wa Haki, Johnston Businge, alipuuza umuhimu wa kuachiliwa kwa Ingabire.

”Hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kuachiliwa kwake na hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kufungwa kwake”, aliliambia shirika la habarila Reuters.

 

 

BBC news