×

ODEMBA APORWA MUME MCHANA KWEUPE!

Miriam Odemba

UBUYU ni miongoni mwa matunda ambayo hayachoshi hasa ukiwa unajua jinsi ya kuumun’gunya ili usichubuke ulimi! Ubuyu mtamu uliotua kwenye meza ya Ijumaa Wikienda unamhusu mwanamitindo maarufu ambaye alitamba miaka ya 90 na kujizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi.  Huyu si mwingine bali ni Miriam Odemba ambaye kwa sasa maisha yake ameyahamishia huko Paris nchini Ufaransa.

APORWA MUME

Kwa mujibu wa mleta ubuyu wetu ambaye yupo karibu na mrembo huyo, Odemba kwa sasa anaishi peke yake huku akimlea mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 8 aliyempa jina la Iris kutokana na mumewe aliyezaa naye kuporwa mchana kweupe na mwanadada ambaye ni mwanamitindo kutoka Kisiwa cha Madagascar.

Msambaza ubuyu huyo alitiririka kuwa baada ya mwanamitindo huyo kugundua hayo aliamua kuinua mikono juu na kuanza kusaka maisha yake peke yake huku akimuangalia mtoto wake mwenyewe huko ughaibuni.

MSIKIE ODEMBA MWENYEWE

Baada ya kupata ubuyu huo Ijumaa Wikienda, kama kawaida yake lilifanya jitihada ya kumtafuta Odemba kwa njia ya simu ambapo aliamua kufunguka kila kitu.

Ijumaa Wikienda: Habari za siku Odemba?

Odemba: Salama kabisa…

Ijumaa Wikienda: Hapa ni Gazeti la Ijumaa Wikienda, kuna mambo nataka kuzungumza na wewe.

Odemba: Daah… kuna kitu gani kwangu leo maana umeniogopesha sana…

Ijumaa Wikienda: Hakuna shida sana ila nitaka kufahamu kuwa huko unapoishi upo na mumeo?

Odemba: Awali nilikuwa ninaishi naye, lakini kwa sasa hivi hapana!

Ijumaa Wikienda: Kuna kitu gani kimetokea maana najua mmezaa mtoto?

Odemba: Unajua mimi kuna mambo mengine ambayo ni ya maisha yangu zaidi na yananihusu mimi, sipendi kuyaweka kwenye vyombo vya habari maana ni binafsi zaidi.

Ijumaa Wikienda: Ila madai yaliyopo ni kwamba ndoa yako uliyofunga kwa mbwembwe ilivunjika baada ya kugundua mumeo ambaye ni mtasha anachepuka nje ndiyo ukaamua kuachana naye, je, madai haya ni kweli?

Odemba: Okey, ngoja niweke wazi hilo maana naona mshapata habari nzima, unajua sasa mimi mara nyingi kazi yangu ni kusafiri safari kwa ajili ya kufanya kazi ya uanamitindo, sasa wakati ninasafiri mwezangu akapata vishawishi na unajua ana jina kubwa sana huku (Ufaransa) ndiyo maana na hata baada ya kugundua hivyo niliamua kukaa pembeni na kulea mtoto wangu mwenyewe.

Ijumaa Wikienda: Sasa huyo aliyekuchukulia mumeo unamjua?

Odemba: Ndiyo, ni msichana ambaye ana mchanganyiko wa Kihindi na Madagascar, maana naona aliona mimi nafahidi sana.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo mpaka sasa upo kwenye mgogoro wa ndoa na huyo mumeo?

Odemba: Ngoja niweke sawa hapo unajua yule ni mzazi mwezangu tu na bado tulikuwa hatujafunga ndoa, lakini sasa hivi kaona hakufanya sawa kwangu hivyo ameanza kurudisha uhusiano mzuri kwangu ambapo tunaweza kuongea kuhusu mtoto wetu na vitu vingi.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo una mpango wa kurudi kwake hivi karibuni?

Odemba: Unajua nilikuwa namfundisha siyo vyema kuchezea wanawake, lakini baada ya muda naamini mambo yatakaa sawa tu.

Ijumaa Wikienda: Huko ufaransa kwa sasa unafanya nini, maana mwanzoni alikupeleka huyo mpenzi wako?

Odemba: Mimi huku nimeshakuwa mwenyeji kabisa bado nafanya kazi yangu ya uanamitindo na pia huku natangaza mavazi ya tamaduni zetu kama vazi la kimasai, watu wengi wanapenda.

Ijumaa Wikienda: Haya Odemba shukrani sana.

Odemba: Karibu sana na hivi karibuni narudi nyumbani kuendeleza kampeni yangu ya Run With Odemba.

MAKALA: Imelda Mtema, DAR