
Yusaku Maezawa ambaye ni mfanyabiashara na mwendesha shughuli za mitindo, atakuwa abiria wa kwanza kwenda kwenye mwezi.
Mtu huyo ambaye ana utajiri wa Dola bilioni 3 (Sh. trilioni 6.8) atapelekwa mwezini mwaka 2023.
Mhusika wa mradi huo aitwaye Elon, ametoa baadhi ya picha za chombo cha Big Falcon Rocket ambacho kitakuwa kinapeleka watu mwezini.
