×

DRAKE AMSHITAKI MWANAMKE ANAYEDAI ALIMBAKA, KUMPA UJAUZITO

MWANAMUZIKI wa Marekani, Drake,   amefungua mashitaka dhidi ya mwanamke anayedai alimbaka na kumpa ujauzito na sasa ana mtoto wake.

Drake amesema katika mashitaka hayo kwamba alikutana na mwanamke huyo, Layla Lace,  mwaka jana, Februari 2017,  katika ziara yake ya muziki iliyoitwa  Boy Meets World Tour huko jijini Manchester, Uingereza, ambapo walifanya mapenzi ya hiari katika hoteli aliyofikia.

Kwa mujibu wa Drake, kilichowafarakanisha ni pale alipokataa kufuatana na mwanamke huyo kwenye ziara yake hiyo na pale alipoacha kujibu meseji alizokuwa anamtumia kwenye simu.

Mwanamke huyo inadaiwa alimtumia Drake meseji za vitisho akisema angefichua siri zake, ambapo alikiambia kituo cha utangazaji cha SiriusXM kwamba mwanamuziki huyo alikuwa amempa ujauzito.

Miongoni mwa meseji ambazo Layla alikuwa anamtumia Drake ni hii hapa chini:

Inasemekana Layla alimtafuta mwanasheria ili aweze kumsaidia katika kupata fedha kutoka kwa Drake kwa ajili ya matunzo ya mtoto anayedaiwa walimzaa.

Katika mashitaka hayo, Drake amekanusha yote hayo na kumtaka Layla amfidie kwa kumwibulia kashfa ya uongo na kudai mamilioni ya fedha kwa kitu ambacho hakipo.