STAA wa filamu nchini Ghana anayefanyia kazi zake Nollywood, Van Vicker, amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jini Dar es Salaam alfajiri ya leo Septemba 27 na kupokelewa na mwenyeji wake, Wema Sepetu.
Katika mahojiano yake na wanahabari, Van Vicker amemwagia sifa za kutosha Wema kwa kazi nzuri anazofanya za sanaa huku akimtaja kwa jina la Tanzania Sweetheart.
Mbali na Wema, Van amemtakja Marehemu Charles Kanumba kama msanii aliyekuwa hana kifani katika tasnia hiyo hapa nchini na kudai kwa sasa anamkubali sana Mzee Hashim Kambi ambaye pia amefanya kazi nyingi za filamu ndani na nje.
Van Vicker amekuja nchini kwa ajili ya kuzindua filamu yake aliyofanya na Wema inayoitwa ‘D.A.D’ inayotarajiwa kuzinduliwa Katika Ukumbi wa Mlimani City kesho Septemba 28 ambapo pia itakuwa ni siku ya kuzaliwa ya Wema Sepetu.