×

WAKAZI AWAPA SOMO WASANII KUHUSU KIKI

Image result for WAKAZI

MSANII wa HipHop Bongo, Webiro Wassira ‘Wakazi’ ameibuka na kuwapa somo wasanii ambao wanapenda kufanya kiki kabla ya kutoa nyimbo zao kwamba licha ya kuwa ni njia mojawapo ya biashara, lakini inapotosha kama kazi ikiwa mbovu.

 

Akipiga stori na Risasi Vibes, Wakazi alisema hawezi kufanya kiki ili ‘kuboost’ wimbo wake ufanye vizuri, lakini atatoa kazi nzuri ambayo ni kiki tosha maana yote yanawezekana hivyo hata wasanii wengine wajitahidi kufanya kazi nzuri ili zijiuze zenyewe.

 

“Wasanii wanaofanya kiki wanatakiwa kuwa makini sana kwa sababu pamoja na kwamba wanaona ni njia mojawapo ya kuuza kazi zao, inaweza ikawaharibia kama kazi wanazotoa ni mbovu mwisho wa siku kiki inageuka maisha badala ya muziki, wafanye kiki wakiwa na uhakika kazi zao ni nzuri,” alisema Wakazi.

SHAMUMA AWADHI