×

MV Nyerere: Gari, Pikipiki Vikiopolewa Majini – Video

ZOPEZI la uokoaji na uopoaji wa Kivuko cha MV Nyerere limehitimishwa leo katika Kisiwa cha Ukara, wilayanai Ukerewe mkoani Mwanza huku wataalam wa uokoaji wakiopoa mali na mizigo iliyokuwa imezama majini kufuatia maafa hayo.

 

Asubuhi ya leo Septemba 29, 2018, wazamiaji wameopoa pikipiki moja na baiskeli, vifaa vya umeme vya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na jana walifanikiwa kutoa gari aina ya Toyota Canter iliyokuwa imezama majini, mikoba ya mikononi, mifuko yenye bidhaa za aina mbalimbali za viatu vya watu wazima na watoto.

 

Aidha, vitu vingine vimeendelea kutolewa leo katika kivuko hicho ambacho tayari kimeshavutwa hadi pwani ya mwalo katika la Kijiji cha Bwisya na zoezi la kukagua iwapo kuna chochote kimesalia limeshakamilika.

Kivuko cha Mv Nyerere kilizama majini Septemba 20 na kusababisha vifo vya watu 230 huku watu 41 wakiokolewa.

TAZAMA VITU HIVYO VIKITOLEWA ENEO LA TUKIO