×

BENKI YA STANBIC YATOA ZAWADI KWA WATEJA

Mteja wa Benki ya Stanbic, Ruth Bura akifurahia kupokea chupa ya kinywaji chake pendwa cha ‘champagne’ kama zawadi kutoka kwa mhudumu wake wa Benki ya Stanbic, Edward Nyerere wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Centre. 
Ruth Bura mteja wa Benki ya Stanbic akifungua chupa ya ‘champagne’ na wafanyakazi wa benki hiyo, Edward Nyerere (kushoto), Jacquiline Michael (wa pili kushoto) na Elikaneny Uloto (kulia) wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika Tawi la Centre. 
Mteja wa Benki ya Stanbic, Aisha Sykes akimshukuru, Fredrick Mushi, mhudumu wake wa benki, baada ya kumpatia ujumbe wa kumshukuru kwa kuwa mteja wa benki ya Stanbic. 
Mshauri wa wateja wa Benki ya Stanbic akimpa mteja wake ujumbe wa shukurani kwa kufanya miamala yake ya kibenki na Stanbic.
Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Centre, Bw. Adelhem Msiagi (kushoto) akimpa mteja wao ujumbe wa shukurani kwa kuchagua kufanya miamala yake ya kibenki na benki ya Stanbic wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Centre.   

 

Benki ya Stanbic imesherehekea wiki hii ya huduma kwa wateja kwa kuwapa zawadi wateja wao na kuwashukuru kwa kuendelea kuwa wateja wa benki hiyo.